المشاركات

𝗞𝗪𝗘𝗟𝗜 𝗞𝗔𝗕𝗜𝗦𝗔 𝗞𝗢𝗖𝗛𝗔 𝗙𝗔𝗗𝗟𝗨 𝗗𝗔𝗩𝗜𝗗𝗦 𝗔𝗠𝗘𝗔𝗠𝗨𝗔 𝗞𝗨𝗢𝗡𝗗𝗢𝗞𝗔 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔 𝗦𝗖.



Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Fadlu Davids ameamua kuachana na klabu hiyo. Fadlu analalamikia mazingira ya kazi, ni kama ana hofu ya usalama kitu ambacho ameshindwa kuweka wazi moja kwa moja. Viongozi wa Simba SC wamejitahidi kumbembeleza abadilishe msimamo wake huo lakini amekataa katakata, Rais wa heshima wa klabu Mohamed Dewji - MO amemaliza mbinu za kumtongoza Fadlu iikiwemo kumuongeza mshahara wake, MO amemtaka Fadlu aseme anataka aongezwe kiasi gani (Open Check) lakini Fadlu anasema ameshafanya maamuzi ya kuondoka na harudi nyuma. 


Viongozi wa Simba wamemuachia yeye Fadlu ndiyo aamue kama ni kuvunja mkataba basi avunje na aje autangazie umma kwamba ameamua kuondoka klabuni hapo. Mwanzo Fadlu alitaka wafikie makubaliano ya pande zote mbili, Simba wamekataa hilo wanajiondoa kuonekana wamemfukuza ilihali ukweli ni kwamba yeye anataka kuondoka.

Inasemekana klabu ya nyumbani kwao Afrika Kusini ya Kaizer Chiefs ndiyo imempagawisha baada ya kumpa ofa kubwa ya mshahara wa dola za Kimarekani 80,000/. Pia Wydad Casablanca imo kwenye mbio za kumrejesha Kocha huyo ambaye kabla ya kuja Simba alikuwa huko. 

Yuko na timu Francis Town lakini amefanya maamuzi ya kuondoka na alitaka hata huko Francis Town asiende aishie Gaborone tu.

إرسال تعليق

NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...