🚨🇹🇿 𝐄𝐗𝐂𝐋𝐔𝐒𝐈𝐕𝐄: klabu ya Simba SC bado haijamaliza usajili — kwani licha ya namba ya wachezaji wa wa kigeni tayari wamejaza nafasi zote 12 za wachezaji wa kimataifa. 💯
Vyanzo vinaeleza: Endapo watampata mchezaji wa kiwango cha juu wanayemlenga, basi kuna uwezekano mkubwa kwamba Lionel Ateba 🇨🇲 au Joshua Mutale 🇿🇲 wataachwa kwenye kikosi. Uamuzi huo tayari umefikishwa ndani ya klabu.
Simba SC wamepokea: — Ofa kadhaa kwa ajiliya Ateba na ofa moja rasmi kwa Mutale, lakini klabu imewajulisha vilabu vinavyovutiwa kuwa “hakutakuwa na kuondoka mpaka mbadala sahihi apatikane.”
📌 Masharti ya kuvunja mikataba ya wachezaji hao wote wawili yanatajwa kuwa “magumu sana,” jambo linalomaanisha kuwa dili halitakuwa rahisi isipokuwa nafasi bora ijitokeze.