المشاركات
...🚨🚨𝗕𝗘𝗞𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗠𝗘𝗟𝗢𝗗𝗜 𝗦𝗨𝗡𝗗𝗢𝗪𝗡𝗦 𝗔𝗧𝗨𝗔 𝗠𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔𝗭𝗜
🚨🇿🇦 DILI LIMEKAMILIKA:
Vigogo wa Tanzania, Simba SC, wamethibitishwa kukamilisha usajili wa Rushine De Reuck (29) kutoka Mamelodi Sundowns. ✅
Amesaini mkataba wa mwaka mmoja, ukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine. ✍️
Rushine ni mchezaji anayefahamika vyema na kocha mkuu Fadlu Davids, baada ya kufanya kazi pamoja katika Maritzburg United.
Anakuja kuimarisha safu ya ulinzi kwa uzoefu, ukomavu na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali. 🛡️
Akiwa na Sundowns, alinyakua makombe 8 — yakiwemo mataji 5 ya ligi. 🏆
Mashabiki wa Simba, mnasemaje kuhusu usajili huu?
Credit; Micky Jnr African Football Journalist 👑
#SokaAfrika | #Sundowns | #SimbaSC | #Usajili