المشاركات

SHUJAA WA STELLENBOSCH HUYU HAPA

KUTOKA KUIPANDISHA STELLENBOSCH DARAJA HADI KUIPELEKA NUSU FAINALI YA KOMBE LA CAF .. 📍 Steven Robert Barker ndio majina yake kamili alizaliwa December 23 ya mwaka 1967 huko Maseru, Lesotho. Ni mchezaji wa zamani wa kandanda wa Afrika Kusini na kocha kwa sasa anayesimamia klabu ya Stellenbosch . Stellenbosch tangu kuanzishwa kwake miaka minane iliyopita ni makocha wawili pekee ndio wameifundisha timu hiyo . Kocha wa kwanza kabisa kukinoa kikosi cha Stellenbosch alikuwa ni Sammy Troughton, forward wa zamani wa vilabu vya Wolverhampton, Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns lakini baadae alitimuliwa kutokana na timu hiyo kupata matokeo yasiyorizisha katika ligi daraja la kwanza, klabu iliachana na Troughton na mikoba yake kuchukuliwa na Steve Barker, ambaye hapo awali alikuwa kocha msaidizi katika kikosi hicho . Steve Barker alikiongoza kikosi cha Stellies kunyanyua kombe la ligi daraja la kwanza la taifa msimu wa 2018|19 na kupanda daraja hadi DStv Premiership, ligi kuu ya soka ya Afrika Kusini, wakiwa kama mabingwa wa ligi daraja la kwanza kitaifa . Mnamo December 2023, Steve Barker alikiongoza tena kikosi cha Stellenbosch ama (Stellies) kushinda shindano lake la kwanza la kombe baada ya kutawazwa mabingwa wa kwanza wa Carling Knockout kufuatia ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya TS Galaxy katika uwanja wa Moses Madhiba mjini Durban . Mnamo April 2025, Stellenbosch chini ya Steve Barker iliweka historia kwa kufika nusu fainali ya kombe la shirikisho la CAF kwa mara ya kwanza kabisa kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa watetezi wa michuano hiyo Zamalek ya Misri na kuwa timu ya pili ya PSL kufika hatua ya nusu fainali katika ushiriki wao wa kwanza wa CAF Confederations Cup, baada ya Marumo Gallants msimu wa 2022|23 . STELLENBOSCH KATIKA PREMIER SOCCER LEAGUE 🇿🇦 TANGU WAPANDE DARAJA . ◎ 2019|20 - Position 10 🅿️ 36 ◎ 2020|21 - Position 14 🅿️ 29 ◎ 2021|22 - Position 04 🅿️ 47 ◎ 2022|23 - Position 06 🅿️ 40 ◎ 2023|24 - Position 03 🅿️ 50 ◉ 2024|25 - Position 03 🅿️ 38 Takwimu za Steve Barker katika michuano yote tangu alipoanza kukinoa kikosi cha Stellenbosch mnamo mwaka 2017 . ◉ 218 - Games ◉ 86 - Wins ◉ 67 - Losses ◉ 65 - D #kennysports #kennymedia

إرسال تعليق

NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...