المشاركات
AL AHLI YAFANYA KUFURU KWA VINICIUS
Klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia wameweka mezani ofa ya kihistoria ya €350 milioni kwa ajili ya kumsajili Vinícius Júnior kutoka Real Madrid.
Ofa hii, inayodhaminiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia, inalenga kuvunja rekodi ya uhamisho wa Neymar ya €222 milioni.
Ingawa Real Madrid ina nia ya kumweka Vinícius kwa muda mrefu, ikijaribu kumshawishi kwa mkataba mpya, mshahara uliopendekezwa bado uko chini ya ule wa Kylian Mbappé, jambo linalowapa Saudi Arabia nafasi ya kumshawishi mchezaji huyo.
Hata hivyo, Vinícius bado hajakubali uhamisho huo, na Real Madrid inaendelea na mazungumzo ya kumwongeza mkataba wake.