Posts

DAMARO CAMARA KUIGHARIMU YANGA

 




 #MICHEZO SIMBA SC Vs MOHAMED DAMARO CAMARA & YANGA SC

Tuliishia kwamba Simba SC hawana shida na uraia wa Damaro wa Kiserikali, passport, card ya NIDA,haki zake kisiasa na kiserikali kama Mtanzania, huku kwenye soka ndiyo shida yao, kuna taratibu za tofauti zilipaswa kufuatwa, hazikufuatwa kwa mujibu wa Simba SC. 


Simba SC wameorodhesha hatua 6 ambazo zinafuatwa katika mchakato wa kuhama Shirikisho kwa mchezaji kwa mujibu wa FIFA, ambazo hazikufuatwa.


Kwa mujibu wa Regulations Governing the Application of the Statutes (RGAS), maombi ya kubadilisha Shirikisho lazima yapelekwe kwa Players' Status Committee (PSC)


Kuna aina 4, lakini nimechukua hii ambayo Damaro inamhusu tu. 

 b) Kwa wachezaji wanaotaka kubadili chama cha soka (association) baada ya tayari kushiriki katika mashindano rasmi, katika ngazi yoyote au aina yoyote ya mpira wa miguu, kwa niaba ya chama kingine (Kifungu cha 9 aya ya 2 ya RGAS)


Mohamedi Damaro Camara ana angukia kipengele (b), kwani akiwa Guinea 🇬🇳 alishacheza vilabu vya HAFIA FC na MILO FC, lakini mwaka 2019 alikuwemo kwenye kikosi cha Guinea cha U17. 


1. Kutuma maombi (FA)

2. Kupitiwa na Katibu wa FIFA

3. Maamuzi ya Players' Status Committee

4. Vigezo vya maamuzi ya PSC

5. Msingi wa maamuzi ya PSC

6. Rufani CAS.


Simba SC wanaenda mbali na kusema kwenye Kanuni, Hadhi na Uhamisho wa wachezaji- RSTP) kifungu cha 9 ukurasa wa 78 na 79 hakikufuatwa kwenye usajili wa Damaro, ambacho kinasem


“Mara tu taarifa zote husika zitakapowekwa na nyaraka za lazima kupakiwa, klabu husika zitapaswa kuthibitisha uhamisho huo katika TMS bila kuchelewa na kabla ya mwisho wa kipindi cha usajili cha chama kipya (kwa kuzingatia masharti ya kipekee yaliyobainishwa katika Kifungu cha 6 cha kanuni hizi)”


FOREIGNER PLAYERS

1. Djigui Diarra

2. Pacome Zouzoua

3. Max Mpia Nzengeli

4. Chadrack Boka

5. Duke Abuya

6. Frank Assinki

7. Prince Mpumelelo Dube

8. Lassine Kouma

9. Allan Okello

10. Laurindo Dilson Maria

11. Buba Jammeh

12. Yao Kouassi Attohoula

13. Mohamed Damaro Camara


Simba inataka Yanga SC ipokwe alama, wanasema Damaro hajasajiliwa KIHALALI ni Raia wa Guinea kısoka. 


#kennymedia #Kennyupdates #kennysports

Post a Comment

NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...