TATU MGONGONI,alivaa Haruna Moshi Shaban maarufu Boban, alifanya matusi sana akiwa na Lunyasi..
Muda ukapita,bwana mdogo aliyechipukia timu ya Simba B,William Lucian maarufu Gallas akaitumia jezi namba 3 na moja ya sababu ya kuivaa jezi namba 3 ikiwa Idol wake alikua Haruna Moshi.
Akatwanga kwa muda wake ulivyomalizika akasepa.
Ikapita muda mrefu pasipo jezi hiyo kuvaliwa na msimu huu wa 2025/26 Jonathan Sowah ndio mchezaji anayevaa jezi namba 3.
Huwenda Sowah akafanya makubwa kama aliyoonesha Haruna Moshi Shaban maarufu Boban..
Mwanzo mzuri mpaka sasa kwa Jonathan Sowah, huyu ni mshambuliaji wa viwango sana.
