Posts

...🚨🚨𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔,𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔 𝗪𝗔𝗞𝗜𝗠𝗕𝗜𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗚𝗔𝗢 𝗬𝗔 𝗝𝗔𝗠𝗜𝗜


 #MICHEZO “Bado Sina taarifa rasmi ya kwamba tumeomba Mchezo wa Ngao kubadilishwa, unajua hapa Simba Kuna idara na taarifa kama hiyo maana yake inaanzia kwenye kamati ya Ufundi kwa hiyo Mpaka sasa na Mimi nimeona tu taarifa mitandaoni”


“Kusema ukweli ukijaribu kuangalia ratiba imekuwa ngumu Sana , maana ratiba ya Ngao ni tarehe 16, kuanzia hapo tutakuwa na Siku tatu au nne inabidi tucheze mchezo wa ligi ya mabingwa Botswana, na kama unavyojua utaratibu wa kusafiri Botswana Huwa ni magumu sana na mara nyingi Huwa tunaenda na Ndege ya kukodi kuepusha usumbufu”


Lakini ukijaribu kuangalia ucheze mechi tarehe 16, hapo hapo inabidi upumzike , halafu usafiri na baadae kati ya tarehe 19 au 20 ucheze Mchezo Unaweza kuona ni kwa Kiasi Gani ni vigumu”


“Kama Mchezo utakuwa tarehe 20 angalau naona Kuna namna tunaweza kukimbizana na mambo tukapangilia mambo yote lakini kama wenyeji wetu watachagua tarehe 19 basi ratiba itazidi kuwa ngumu zaidi” - Ahmed Ally akizungumza na EFM


Post a Comment

NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...