Afisa habari wa Singida Big star Hussein Masanza amesema Hakuna biashara yoyote iliyofanyika kwa klabu ya Simba kumsajili mshambuliaji huyo kwani walima alizeti hao wamewapa mchezaji bure kabisa na kama ingekuwa kumuuza hakuna klabu nchini ambayo ingeweza kumsajili kwani thamani yake ni bilioni 2.6
"Kama taarifa inavyoeleza ni makubaliano kati ya mlezi wetu Dk Mwigulu Nchemba na Rais wa Simba Mohamed Dewji na kisha kuidhinishwa na uongozi wa Singida Big star, naweza kusema ni kama fair play kama unavyojua Mh Mwigulu ni kiongozi wa watu wote, Simba hawajalipa kiasi chochote cha pesa
Dk Mwigulu amekuwa na mchango mkubwa kwenye soka letu, ameushawishi uongozi na uongozi ukaona ni jambo jema, watanzania wasifikiri niliwadanganya kwamba Tanzania hakuna klabu ingeweza kumnunua, kwasababu thamani ya Sowah ni dola milioni 1 sawa na billion 2.6 kwa pesa za Tanzania, kwamba kwasababu nilisema nilisema hivyo basi imefanyika hivyo, hakuna biashara yoyote, hakuna pesa yoyote ambayo Singida tumepokea kutoka Simba, kwasababu Sowah ni mchezaji professional, tuliwaambia Simba wakubaliane na mchezaji na baada ya kukubaliana basi sisi tulimruhusu, nimpongeze mlezi wetu Mh Mwigulu Nchemba kwa kuwa kiongozi wa mfano lakini sisi pia tunaona ni fursa ya kuboresha mahusiano na klabu nyingine" alisema Masanza