Posts

...🚨🚨🚨𝗧𝗔𝗝𝗜𝗥𝗜 𝗔𝗠𝗘𝗦𝗛𝗔𝗦𝗘𝗠𝗔 ,𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔 𝗠𝗣𝗬𝗔 𝗜𝗡𝗔𝗞𝗨𝗝𝗔

NAJUA MIOYO YA WANASIMBA IMEBEBA MASWALI MENGI - MO DEWJI

Anaandika Muwekezaji wa Klabu ya Simba SC Mohamed Dewji>/h> "Najua mioyo yenu imebeba maswali mengi. Kama Rais wenu, msione nimekaa kimya wakati tumepitia kipindi hiki kigumu. Kupambania Simba ni wajibu wangu>/h> Huu siyo wakati wa lawama — ni wakati wa kusimama imara, kuwa kitu kimoja, na kuchukua hatua sahihi za kuleta mabadiliko chanya. Katika siku chache zijazo, nitazungumza na nyie moja kwa moja. Kuna kazi kubwa inaendelea, na kuna matumaini ya kweli. Simba haijapotea. Tumekuwa kwenye kipindi cha mpito — tumejenga kikosi kipya, tumeimarisha benchi la ufundi, na tumeweka msingi wa mwelekeo mpya. Msimu huu tumefika mbali zaidi ya matarajio, na msimu ujao tunarudi kwa nguvu mpya. Naomba tuendelee kuwa wavumilivu. Tunahitaji kufanya marekebisho makubwa. Tuendelee kusimama pamoja kama familia moja. Mbele yetu kuna mwanga. Na kwa pamoja, tutarudi tukiwa imara zaidi, wenye njaa zaidi, na wa kishujaa zaidi" ameandika MO Una maoni gani?

Post a Comment

NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...